Huku kura zikiendelea kuhesabiwa nchini Mexico
inaelekea chama cha mapinduzi cha rais Enrique Pena Nieto, kinaelekea kupata
ushindi licha ya hasira za wapigaji kura kwamba, uongozi huo haujapambana na
kumaliza vitendo vya uhalifu mkubwa nchini humo na vilevile kashfa za kisiasa.Kumekuwa na
vitendo vya kujaribu kuvuruga kura hiyo na hata baadhi ya wapiga kura kuisusia.
Baadhi ya wapigaji kura wameelekeza hasira zao kwa kuchoma karatasi za kura.
Ilibidi maafisa wanaosimamia uchaguzi
katika jimbo la Guerrero kusitisha zoezi hilo baada ya kukabiliwa na wazazi wa
wale wanafunzi 43 waliopotea katika mazingira tata.Karatasi za kupigia kura pia zilichomwa
katika majimbo ya Chiapas na Oaxaca, na ilibidi vikosi vya walinda usalama
kuingilia kati.Tangu wiki jana
kumekuweko na maandamano yaliyoongozwa na chama cha walimu wanaodai mageuzi ya
kuboresha secta ya elimu nchini humo.
0 comments:
Post a Comment