Katibu Mkuu wake Bwana
ABDULRHAMAN KINANA amesema chama hicho hakijazuia wagombea wa nafasi mbalimbali
za uongozi kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu kushiriki kwenye midahalo mbalimbali
kwa lengo la wananchi kuwasikiliza wagombea na kuwapima.
Kauli yake inakuja siku moja
baada ya chama kutoa tamko la kuzuia midahalo kwa wagombe wake ambao wataalikwa
kwenye midahalo inayoandaliwa katika
kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo wagombea wanapita kwa wananchi
kuomba kuwadhaimini kwa nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.
Lakini Bwana KINANA amewasihi
wanaondaa midahalo hiyo, watoe fursa sawa na kutenda haki wakati wa kuendesha
midahalo hiyo na kutaka isitumike kuleta mifarakono isiyo na sababu,lengo
likiwa ni kuwafahamu wagombea na kusikiliza sera zao na kupima uwezo wao ili
watanzania wapate nafasi ya kuwapima na kufanya maamuzi.
Wakati huo makada zaidi wa chama
hicho wameendelea kujitokeza kutangaza nia yao ya kuwania urais akiwemo Waziri
wa Maliasili na Utalii LAZARO NYALANDU na hapo kesho Waziri wa Mambo ya Nchi za
Nje BERNARD MEMBE naya anatarjia kutangaza nia hiyo.
0 comments:
Post a Comment