Inadaiwa kuwa lengo lao ni
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa
elektroniki BVR kwa ushawishi wa kutoa rushwa kwa maafisa wa uandikishaji na
watendaji wa serikali za vijiji na vitongoji.
Hayo
yamebainishwa na afisa
muandikishaji jimbo la Kyerwa Bwana GEORGE MKINDO wakati akizungumza
hilo amesema ofisi yake kwa kushirikiana na vyombo vya usalama
vimejipanga kuwadhibiti wahamiaji haramu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM
wilaya ya Kyerwa Bi.ODILIA MAHOLELO na Naibu Katibu wa Baraza la Vijana CHADEMA
wilaya ya Kyerwa Bwana EVODIUS KATARAMA wametaka wenyeviti wa serikali za mitaa
na mawakala wa vyama vya siasa kushirikiana na tume ya uchaguzi kuwadhibiti
wahamiaji kujiandikisha kwenye daftari la uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment