Wakati wa kuzindua ombi hilo la changisho
mjini Brussels, Ubelgiji, Msaidizi wa Katibu Mkuu na Naibu Mratibu wa Masauala
ya Kibinadamu, Kyung-Wha Kang, amesema zaidi ya raia milioni 8 wa Iraq sasa
wanahitaji misaada na ulinzi wa dharura.
Amesema ingawa Umoja wa Mataifa na wadau wa
kibinadamu wamekuwa wakitoa misaada, programu za utoaji misaada sasa
inakabiliwa na upungufu wa ufadhili, na hivyo kutishia kukatiza asilimia 50 ya
jitihada za utoaji misaada.
Msemaji wa changisho hilo ni Simon Ingram,
ambaye ni Msemaji Mkuu wa shirika la UNICEF, ukanda wa Mashariki ya Kati na
Afrika Kaskazini
"Changisho hili linalenga tu kufadhili
mahitaji ya dharura, ya kuokoa maisha ya watu wapatao milioni tano na nusu kwa
miezi sita ijayo. Kuna upungufu mkubwa sasa, kwa hiyo zinahitajika kwa sababu
baadhi ya huduma muhimu, kama za afya na chakula, zinakwama na hata kufungwa
kwa sababu fedha zinakwisha."
Tayari kliniki 77 muhimu zimefungwa na mgawo
wa chakula kupunguzwa kwa zaidi ya watu milioni moja.
0 comments:
Post a Comment