Amesema hayo wakati akifungua jukwaa la
kimataifa la kilimo katika maonyesho ya Milan,EXPO Milano 2015 linalofanyika
wakati huu ambao ni hitimisho la miaka 15 ya kumaliza njaa na duniani na
kuanza kwa lengo jipya endelevu la kutokomeza kabisa njaa na kufikia uhakika wa
chakula na lishe.
Kwa mantiki hiyo Da Silva amesema mafanikio
yamepatikana kwa lengo la milenia lakini anarejelea wito kwa washiriki kufikia
lengo jipya safari inapoanza ya kutekeleza.
Bwana Da Silva amesema msingi wa njaa siyo
uhaba wa chakula bali umaskini ambao unachochewa na ukosefu wa usawa na
unajikita katika masuala ya ukosefu wa maji, ardhi, masoko na zana nyingine za
uzalishaji
Amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake
unatoa msaada wa dhati kwa zaidi ya nchi 100 Afrika, Amerika ya Kusini na Asia
ambazo tayari zimejizatiti kutokomeza njaa.
0 comments:
Post a Comment