Wang amesema hayo katika mkutano usio
rasmi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola.
Amesema, kazi muhimu zaidi kwa sasa ni kusaidia nchi
zinazoathiriwa na ugonjwa huo kurejesha uchumi wao, kuimarisha mfumo wa afya ya
umma, na kuanza ushirikiano katika udhibiti wa magonjwa, utoaji wa mafunzo na
utafiti wa dawa. Amesema, China inajadiliana na nchi husika na Umoja wa Afrika
kuhusu mpango wa kuanzisha "kituo cha kudhibiti na kuzuia ugonjwa cha
Afrika".
Pia China imechangia dola za marekani milioni 6 kwa mfuko wa
kupambana na Ebola wa Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment