Image
Image

Waziri mkuu wa China ataka juhudi zifanyike katika kuokoa watu waliokuwa ndani ya meli iliyozama katika mto Yangtze.


Waziri mkuu wa China Li Keqiang ametaka juhudi zote zifanywe kuwaokoa watu waliokuwa ndani ya meli iliyopinduka na kuzama jana usiku kwenye mto Yangtze baada ya kukumbwa ghafla na kimbunga.
Meli hiyo ilikuwa na abiria 458 wakati ajali hiyo inatokea.
Li anasema, "Jukumu la kwanza ni kuokoa watu, meli imepinduka lakini hatuwezi kuondoa uwezekano kuwa hakuna watu wanaoweza kuokolewa, ndiyo maana ni lazima kutumia nguvu zote katika uokoaji wa watu hao wakiwemo wazee na watoto."
Habari zinasema hadi sasa, watu 15 wameokolewa, wengine watano wamethibitishwa kufa, na zaidi ya 430 bado hawajulikani walipo.
Ajali hiyo inadhaniwa kuwa ni mbaya zaidi kushuhudiwa nchini China kwa miongo kadhaa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment