Bi. Rehema Gwaya ambaye amelazwa katika Hospitali ya
mkoa Songea akiwa na mwanae wa miezi saba anasema chanzo cha kufanyiwa ukatili
huo ni kutofautiana na mke mwenzake aitwaye Zefania Chimgege baada
ya kuhoji masuala ya usafi ambapo Zefania aliyekuwa akipika maandazi
akamwagia karai la mafuta ya moto usoni.
Baada ya kufanyiwa unyama huo shemeji yake ambaye ni
mume wa Zefania Bw.Hafidhi Hamidu Mbaya akamwambia atoke nje ammalizie kwa
kumchoma na kisu.
Mganga mfawidhi katika hospitali ya mkoa Songea(HOMSO)
Dkt.Benedikt Ngaiza anaelezea hali ya mgonjwa huyo huku wakazi wa
songea wakilaani ukatili huo.
Rehema Gwaya na Zefania Chimgege wameolewa sehemu
moja na wote wanaishi katika nyumba ya baba Mkwe na waume zao na
kwamba zefania chimgegeanashikiliwa na polisi kwa kufanya ukatili huo.
0 comments:
Post a Comment