Kwa mujibu wa kanali
hiyo, raia wa Marekani hawana imani na Clinton na kwamba suala hilo liko wazi
sana. Uchunguzi uliofanywa na televisheni hiyo unaonyesha kwamba,
asilimia 57 ya wananchi wa Marekani wana mtazamo hasi na shakhsia huyo,
huku asilimia 52 ya nyingine ikimtaja kuwa asiyeyapa umuhimu matatizo ya raia
wa kawaida.
Aidha uchunguzi huo
umeongeza kuwa, raia wengi wa Marekani hawakuridhia utendaji kazi wa waziri
huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani mwaka 2012 suala ambalo limepunguza
uungaji mkono wa wananchi kwake.
Hii ni katika hali
ambayo uchunguzi wa hapo kabla wa kanali hiyo ya televisheni, ulikuwa
umemtangaza bibi huyo kuwa mwenye mvuto kwa ajili ya mchuano wa uchaguzi wa
mwaka 2016 nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment