Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa
Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR likisema kama hiyo haitoshi misaada ya
kibinadamu kwa watu Laki Sita na Nusu haiwezi kuwafikia kwa kuwa mashirika ya
misaada yamelazimika kujiondoa.
Kwa mantiki hiyo wakimbizi wamemimnika
nchi jirani ikiwem 30,000 Sudan, 15,000 Ethiopia na hivyo kufanya idadi ya
wananchi waliokimbilia nje ya nchi yao tangu mzozo kuzuka Disemba 2013 kufikia
550,000 huku Milioni Moja na Nusu wakisalia wakimbizi wa ndani.
Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR Geneva
anasema wajiandaa kwa hali mbaya zaidi kwa kuwa..
(Sauti ya Adrian).
"Wakimbizi wanataja
ongezeko la mapigano na ukosefu wa uhakika wa chakula kuwa sababu za
kukimbia makazi yao. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu Milioni Tatu nukta Nane
ambao ni Theluthi moja ya wananchi wote Milioni Kumi na Moja wa Sudan Kusini hawana
chakula cha kutosha."
UNHCR inasema pamoja na idadi ya wakimbizi
wa Sudan Kusini kuongezeka, ina hofu pia na mchango wa ombi maalum la usaidizi
wan chi hiyo kwa mwaka 2015 ambalo hadi sasa limechangiwa kwa asilimia 10 tu.
0 comments:
Post a Comment