Viongozi hao pia wamekubali kwamba nchi tajiri
zinapaswa kuzisaidia nchi masikini haswa barani Afrika, kuendeleza teknolojia
safi na kukubali mabadiliko ya tabia nchi ambayo hayaepukiki.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya mazingira ameyaelezea
makubaliano hayo kama ni kuhama katika matetemeko ya ardhi. Ameongeza kuwa
matokeo chanya ya mpango wa dunia yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya
tabia ya nchi uliofanyika mjini Paris mwezi Desemba, sasa yaonekana kudhihirika
zaidi.
Kansla wa Ujeruman Angela Merkel, amesema viongozi
wa nchi zinazounda kundi la G7 wamekubaliana kufuata hatua mbalimbali ili
kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza baada ya mjadala huo, Merkel amesema
kwamba kulikuwa na makubaliano ya kuendeleza ongezeko la joto kwa nyuzi joto
mbili ya nchi ambazo hazijakuwa kiviwanda.
Merkel ameongeza kuwa, suala hili lingejadiliwa kwa
kiwango kikubwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wa umoja wa mataifa
mwezi Disemba huko mjini Paris.
"tunataka kanuni zenye nguvu katika
makubaliano. Hatuna kanuni zenye nguvu kwa sasa ndio maana hilo litakuwa agenda
huko mjini Paris.Tunataka kuhakikisha kwamba nchi zote zipo kwenye nafasi ya
maendeleo ili wastani wa joto iwe chini ya digrii mbili. Kwa maneno mengine ni
kwamba makubaliano yatahusu mjadala kuhusu digrii mbili. Unajua swala hili
litamaanisha kupungua hewa ya sumu duniani kote, na tumekubali kwa namna kwamba
katika mwendo wa karne hii tunataka kuona na tunahitaji kuondoa gesi ya kabon
ya uchumi wa dunia" alisema Merkel.
Kwa upande wake rais Barack Obama amesema, mapambano
dhidi ya wanamgambo wa Islamic State yatafanyika kwa kiwango kikubwa nchini
Iraq.
Akizungumza katika mkutano huo, rais Obama ameelezea
umuhimu wa kuwashirikisha waislamu wa Sunni kwenye mapambano dhidi ya I-S
katika kiini chake, huku akisema kuwa uvamizi wa kijeshi unapaswa kwenda
sambamba na siasa.
0 comments:
Post a Comment