Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akiwasilisha hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa wizara yake katika kipindi cha 2015/2016.
Lukuvi alisema migogoro mingi kati ya
wananchi na wamiliki wa mashamba, wananchi na hifadhi za Taifa imepungua baada
ya mipaka kurekebishwa.
“Rais amefuta umiliki wa shamba la Ufyomi
Galapo Estate na kazi inayoendelea kwa sasa ni kuhakiki, kupima na kumilikisha
ardhi kwa wananchi ili waweze kuitumia,” alisema Lukuvi.
Aliyataja mashamba mengine kuwa ni Utumaini
la Halmashauri ya Wilaya ya Mafia lenye ukubwa wa ekari 4,040 pamoja na shamba
la Malonje katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Waziri Lukuvi alisema bado kuna changamoto
nyingi za mashamba ambayo wananchi wanataka umiliki wake ufutwe.
Kuhusu umilikaji wa ardhi, alikiri bado kuna
tatizo katika maeneo mengi nchini ambayo licha ya viwanja kupimwa, bado
halmashauri zinashindwa kuandaa michoro na hati za kuwapa wananchi wanaohitaji
viwanja hivyo.
Akizungumzia Mji wa Kigamboni katika Jiji la Dar
es Salaam, alisema wizara baada ya kuchunguza imeona kuna haja ya kupunguza
eneo hilo baada ya marekebisho ya Tangazo la Serikali.
“Eneo la mpango limepunguzwa kwa kuondoa kata
tatu za Mpiji, Pembamnazi na Kisarawe ambalo lina ukubwa wa hekta 44,440 ambazo
hazikuwapo katika mpango wa awali, hivyo kubaki na kata sita zenye ukubwa wa
hekta 6,494,” alisema Lukuvi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira, James Lembeli aliitaka Serikali kusimamia kauli yake
kwamba haiwezekani kupima ardhi kama haijawalipa fidia wamiliki wa maeneo hayo.
Lembeli alisema mpango wa Serikali kutwaa
ardhi ya wananchi bila kulipa fidia unatakiwa ukomeshwe na kutolewa maelekezo
kwa taasisi zote kuacha kufanya uthamini utakaoidhinishwa na mthamini mkuu
kabla halmashauri au mlipa fidia kuthibitisha kama ana fedha za kulipa.
“Kuna maeneo mengi ambayo wananchi
wamechukuliwa maeneo yao bado hawajalipwa fidia.
0 comments:
Post a Comment