Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye akitazama kina cha eneo la kuhifadhia maji wakati Katibu Mkuu
wa CCM,Abdulrahman Kinana alipofika kukagua ukarabati mkubwa uliofanyika
kuufufua mradi wa maji wa Nshamba, wilayani Muleba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akifungua maji, alipotembelea mradi wa maji wa Nshamba, wilayani Muleba mkoani Kagera, ambao umefanyiwa ukarabati mkubwa kuufufua, baada ya kufa zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiwa amezungukwa na umati wa wananchi,alipohutubia mkutano wa hadhara, jana, Juni 8, 2015,katika mji mdogo wa Nshamba,jimbo la Muleba Kusini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua chumba cha kompyuta katika shule ya sekondari ya Nyakatanga, wilayani Muleba mkoani Kagera, jana, Juni 8, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma za asili alipopokewa kwa ngoma, katika Kijiji cha Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera, jana Juni 8, 2015.
Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge wa muleba Kaskazini, Mwijage wakiteta jambo wakati wa mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika Izigo, jana, Juni 8, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa makatibu wa CCM wa kata zilizomo jimbo la Muleba Kaskazini wakati wa mkutano uliofanyika Izigo, jana Juni 8, 2015. Kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Charles Mwijage.
Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akimpa maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu mradi wa mabwawa ya ufugaji samaki, alipokagua mradu huo, jana, Juni 8, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,akishirikiana na baadhi ya viongozi na wananchi kuvuta waya wa umeme, kusaidia katika utandazaji nyaya katika mradi wa umeme unaofanyika katika Kijiji cha Nyakatanga, wilayani Muleba mkoa wa Kagera, Kinana alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa huo, jana, Juni, 8, 2015. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongela na Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka (watatu kulia).
0 comments:
Post a Comment