Image
Image

Rais FRANCOIS HOLLANDE Anaanza ziara nchini Algeria leo.


Rais FRANCOIS HOLLANDE wa Ufaransa , leo anaanza ziara  nchini Algeria  iliyokuwa zamani adui mkubwa wa  nchi yake ili nchi hizo mbili zishirikiane kwa karibu kusaidia k umaliza machafuko ya kisiasa na  tishio la jihadi kwa nchi za Mali na Libya.
Ziara hiyo itakuwa ya pili kwa Bwana HOLLANDE ba ada ya ile ya mwaka 2012 ambayo  alitambua karne ya utawala wa kikatili wa Ufaransa kwa watu wa Al geria uliomalizika kwa vita vya  umwagaji damu kwa uhuru wa nchi hiyo.
Wakati bado kuna masuala nyeti kati ya nchi hizo mbili kama kukataa  kwa Bwana HOLLANDE kuomba radhi  kwa uhalifu uliofanywa na utawala wa kikoloni wa nchi yake kwa  Algeria wasi wasi wa pande zote  kuhusu kushamiri itikadi ya jihadi kaskazini mwa Afrika ambayo imepewa kipaumbele na pande zote.
Algeria inapakana na Mali ambayo bado iko katika hali tete baada  ya oparesheni ya Ufaransa mwaka juzi  kuwatimua wapiganaji wa jihadi waliokuwa wamekamata nusu ya ma eneo ya kaskazini ya taifa hilo  la Afrika Magharibi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment