Siku ya Mtoto wa Kike ambayo kauli yake mbiu mwaka huu ni “Miaka 25 Baada ya Kupitishwa kwa Mkataba wa Haki za Mtoto wa Afrika: Kuongeza Kasi na Jitihada Zetu za Pamoja Kutokomeza Ndoa za Utotoni Afrika” kwani ni ukiukwaji wa haki za mtoto wa kike kutokana na kuwa ndoa nyingi zinapangwa na kujikita zaidi katika makubaliano kati ya anayetaka kuoa na wazazi wa mtoto wa kike na kushindwa kuhakikisha mhusika mkuu anaridhika.
Ndoa za umri mdogo zimeonyesha kuongezeka kwa kipindi cha
miaka kumi iliyopita ambapo takwimu zinaonyesha kuwa bara la Afrika na Asia
vitendo hivyo vinaongoza.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Watu na Afya nchini
Tanzania (TDHS) wa mwaka 2010, wastani wa watoto 4 katika kila watoto 10 wa
kike wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 na inakadiriwa kuwa asilimia
37 ya wanawake wa umri kati ya miaka 20 na 24 kwa mwaka 2000 – 2011 waliolewa
au kuwa na mahusiano ya ndoa walipofikia umri wa miaka 18.
Aidha kwa mikoa ya Tanzania imeonyesha kuwa ndoa za umri
mdogo zinaogoza katika mikoa ya Shinyanga (59%), Tabora (58%), Mara (55%) na Dodoma (51%) ambapo
kisiwani Pemba imeonyesha kuwa katika kila watoto 10 wanaokwenda shule, watano
hawamalizi masomo yao kutokana na kuolewa.
Sababu za kuendelea kwa
ndoa za utotni nchini Tanzania ni Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ambayo inaruhusu
watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 kuolewa kwa ruhusa ya mahakama, na wenye
umri wa miaka 15 kuolewa kwa ridhaa ya wazazi wao, sheria za kimila za baadhi
ya makabila kutoa maamuzi ya ndoa kulingana na mila na desturi zao.
Aidha sababu zingine ni ndoa za umri mdogo
kujitokeza zaidi katika maeneo yenye familia masikini, mila na desturi
kandamizi ambapo kwa utafiti wa Utu wa Mtoto wa Kike ( Child Dignity Forum-
CDF), watoto wa kike wanaotoka kwenye kaya masikini wana uwezekano wa kuolewa
mara mbili zaidi kabla ya umri wa miaka 18 ikilinganishwa na kaya zenye uwezo
TAMWA inaamini kuwa wadau mbalimbali hapa
nchini na duniani wakishawishi hatua za kushughulikia mahitaji ya watoto hasa
wa kike kwa kuelekeza nguvu kwa wahusika wote pamoja na kuondoa vikwazo vyote
vinavyozuia kufikiwa kwa haki hizo, ndoa hizo zitapungua kama siyo kuisha
kabisa.
0 comments:
Post a Comment