Taasisi ya Masuala ya Kimataifa
ya Afrika Kusini imesema kama
inavyofahamika Umoja wa Afrika unafanya
mkutano wake hapo eneo ambalo limetangazwa kama
eneo la Umoja huo kwa mujibu wa
kanuni za kimataifa.
Kwa sababu hiyo msemaji wa
taasisi hiyo,Bwana HOPEWELL RA DEBE
amesema polisi wa Afrika Kusini hawawezi kwenda mahali hapo na kumkamata mtu
yeyote wakati wa kipindi cha mkutano huo ulioanza jana na unatarajia kukamilika leo.
Amesema Serikali ya Afrika Kusini ilijua hali hiyo kwamba suala la Rais BASHIR lingeibuliwa na mashirika ya kimataifa na makundi mengine ya
ushawishi na ndiyo ime jitokeza Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya ICC ambayo imekuwa inamtafuta
kwa muda mrefu ku taka Afrika ya Kusini ambayo ni mwanachama wa mahakama hiyo imkamate kitu
ambacho hakiwezekani.
0 comments:
Post a Comment