Ugonjwa huu ni kati ya magonjwa ambayo huwasumbua wanawake mara kwa mara.
Miongoni mwa njia ambazo huchangia kuambukiza kwa ugonjwa huu ni pamoja na matumizi ya vyoo vichafu na kuchangia nguo za ndani pia.
Mbali na hayo joto pamoja na unyevu mwingi na nguo za kubana pia huweza kuchangia kutokea kwa fangasi hizi za sehemu za siri (ukeni)
Mbaya zaidi ugonjwa huu huweza kuambukizwa kwa njia ya ngono endapo mhusika mwenye tatizo hili atakutana kimwili na mwenza wake ambaye hana maambukizi bila kutumia kinga.
Fangasi huweza kuwa na dalili zifuatazo:
Kuwashwa sehemu za siri hasa kwenye uke na sehemu za mashavu ya uke.
Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo wakati mwingine huweza kuwa na harufu.
Kupatwa na maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa.
Ili kuepuka kupata ugonjwa huu inashauriwa kuvaa nguo za ndani zilizokauka vizuri na kuzingatia usafi wa sehemu za siri na kujikausha vizuri mara baada ya kuoga pamoja na kuimarisha usafi wa choo.
0 comments:
Post a Comment