Siku hii pia inatumiwa kuwakumbuka wakenya
waliopigania uhuru wa nchini hiyo miaka ya hamsini na sitini kabla ya
kujinyakulia uhuru chini ya vuguvugu la Mau Mau.
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihotubia taifa
katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Maadhimisho ya mwaka huu yanakuja wakati nchini hiyo
ikikabiliana na changamoto za usalama kutokana na vitisho vya kundi la
wanamgambo wa kiislamu la Al Shabab kutoka nchini Somalia.
Hivi karibuni kulitokea makabiliano makali kati ya
vyombo vya usalama na wanamgambo wa Al Shabab. Makabiliano hayo yalitokea
Jumatatu usiku Mei 25 , Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Kijiji cha Yumbis na
maeneo mengine yaliyopembezoni katika Kaunti ya Garissa, yamekua yakilengwa na
wanamgambo hao wa Al Shabab.
0 comments:
Post a Comment