Profesa LIPUMBA ametoa rai hiyo wakati akiwahutubia
wananchi mjini Tabora, akiwa katika ziara ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,
Akizungumzia changamoto zinazowakabili walemavu wa
ngozi albino na kuishi bila amani katika nchi yao, amesema serikali haijatoa
msimamo wa kuwanusuru na janga la kuwindwa kama wanyama.
Wakizungumzia changamoto zinazowakabili wananchi wa
mkoa wa Tabora baadhi ya viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi mkoani humo
wamesema mabadiliko ya wananchi wa tabora yataletwa na wakazi wa Tabora wenyewe
kwa kufanya uamuzi sahihi katika uchaguzi mkuu ujao.
0 comments:
Post a Comment