Image
Image

MWINGULU:Serikali haijasamehe ada ya leseni za mwaka kwa chombo chochote cha usafiri.


Serikali imesema haijasamehe ada ya leseni za mwaka kwa chombo chochote cha usafiri yakiwemo magari, matrekta, pikipiki na vingine ambavyo haviko barabarani kwa sababu yoyote.
Naibu Waziri wa Fedha Mheshimiwa MWIGULU NCHEMBA amesema hayo bungeni wakati akijibu swali lililohoji sababu za magari au matrekta mabovu kuendelea kudaiwa leseni kwa kuwa hayatumiki.
Amesema kwa kuzingaatia sheria hiyo inashauriwa kwamba wamilki wa vyombo vya moto ambavyo ni vibovu na havitumiki waende katika ofisi za Mamlaka ya Mapato ili kufuta usajili wa vyombo hivyo.
Aidha, amesema kama mmiliki atafanya hivyo hataendelea kutozwa ada ya leseni ya kila mwaka kwa kipindi chote ambacho chombo chake hakitumiki.
Hata hivyo, amesema matrekta hayalipiwi ada ya leseni ya mwaka kutokana na umuhimu wake kwa wakulima.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment