Image
Image

Tamasha la Ngoma za Kisukuma lafana Simiyu.


Tamasha la Ngoma za Kisukuma maarufu kwa jina la MBINA ambazo hufanyika kila tarehe 31 ya mwezi mei kila mwaka limefanyika mkoani Simiyu na kufana sana huku wananchi wa mkoa huo wakihimizwa kuendeleza utamaduni wa kabila hilo.
Mashindano hayo ambayo huyakutanisha makundi mawili hasimu ya Wagika na Wagalu yamefanyika kwenye viwanja ya CCM na halimashauri ya mji wilayani Bariadi na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Wakiongea mara baada ya kumalizika kwa ngoma hiyo baadhi ya wananchi waliohudhulia ngoma hiyo wamewahimiza wanananchi wa mkoa huo kuendelea kuuenzi utamaduni wa mila za kisukuma  kwa faida ya vizazi vijavyo.
Wananchi hao wamesema utamaduni huo hauna budi kuenziwa kwani ndiyo njia pekee ya kuwakutanisha wasukuma na kubadilishana mawazo kwa njia ya ngoma huku wakitafakali namna ya kuanza msimu mpya wa kilimo
Katika tamasha hilo hilo kundi la Wagika limeibuka mshindi kwa kuwashinda wenzao wagaru na kupewa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha na Ng’ombe.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment