Wakazi wa kijiji cha Huyum, Wilaya ya Askira-Uba, Jimbo la Borno
ambacho wiki za hivi karibuni kimekumbwa
na mashambulio wanasema k atika shambulio hilo wapiganaji walifyatua risasi ovyo na kuchoma moto mamia
ya nyumba.
Mmoja wa wakazi hao aliyekimbilia jimbo jir ani la Amadawa amesema
wavamizi waizunguka kijiji hicho na
kufyatua risasi na n dani ya kijiji ambako walimwaga mafuta kwenye nyumba 500 za udongo
zilizoezekwa nyasi na kuzichoma m o to.
Shambulio hilo lilikuja wakati wakuu wa majesh i kutoka Nigeria na
nchi jirani wakikutana kuandaa mipango
ya kukiangamiza kikundi h icho ambacho katika mashambulio yake katika miaka sita iliyopita kimeua zaidi
ya watu 15,000.
Mipango hiyo ya wakuu wa majeshi itajadiliwa kesho na viongoz i
Nigeria, Cameroon, Niger na Chad na kwa mara ya kwanza rais wa Beni n naye pia
amealikwa kuhudhuria kikao hicho chenye
nia ya kuanzisha kikosi cha pamoja kuangamiza kikundi hicho.
0 comments:
Post a Comment