Kadhalika, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ametajwa kuwa
ndiye kiongozi wa siasa aliyeshuhudiwa na wananchi wengi katika hotuba
zake kuliko wanasiasa wengine waliokwisha kutangaza nia.
Hayo yamo katika ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la
Maendeleo la Utafiti la Elimu (Tedro), iliyozinduliwa jijini Dar es
Salaam jana.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob
Katerri, alisema ripoti hiyo ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu
2,000 kutoka vijijini na mijini.
Alisema katika ripoti hiyo kipengele cha watangaza nia
walioshuhudiwa na watu wengi katika hotuba, Lowassa anaongoza kwa
kushuhudiwa kwa asilimia 54, akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (46), Naibu Waziri wa Fedha ,
Mwigulu Nchemba (44), Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven
Wasira (40) na Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani(39).
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba(34), Waziri
Nchi Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (31), Mbunge wa Bunge la
Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (27), Waziri wa Ujenzi, John
Magufuli (23), na Mbunge wa Sengerema, Willium Ngeleja (19) na wengine
wakifuata.
Katika Kipengele cha kupunguza tatizo la ajira, ripoti hiyo
ilieleza kuwa wananchi walipohojiwa walieleza kuwa wana imani na Lowassa
kwa asilimia 19, Nchemba (14), Magufuli (13).
Makamba (13), Membe (12), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (10),
Mwandosya (7), Dk. Harrison Mwakyembe (7), Wassira (2) na wengine (3).
“Utafiti huu umebaini kuwa watangaza nia wengi pamoja na mambo
mengine walijikita sana katika kusema watatatua tatizo la ajira kwa
vijana,” alisema Kaserri.
Kadhalika ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha kuinua elimu
nchini, ambacho wananchi waliohojiwa walitoa nafasi kubwa ya uwezekano
wa kutekelezewa kwa kipaumbele hiki kwa Lowassa kwa asilimia 25.
Nchemba (18), Membe (16), Makamba (13), Magufuli (12), Mizengo Pinda (12), Wasira (3) na wengine (9).
Pia ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha Tanzania kuwa nchi ya
kipato cha kati ifikapo waka 2025, na wananchi walikuwa na imani na
Nchemba kwa asilimia 13.4 kuwa ataweza kulipeleka taifa kufikia kipato
cha kati.
Lowassa (11), Wasira (9), Membe (9.20), Magufuli (9.0), Makamba
(5.3), Mwandosya (4.60), Pinda (3.5) na Dk. Mwakyembe (1.40).
Hata hivyo, utafiti huo ulielezea kipengele cha kuinua sekta ya
Kilimo na Mifugo nchini ambacho kwa watangaza nia hao, wananchi walikuwa
na imani kwa Pinda kwa asilimia 23.
Lowassa (17), Nchemba (16), Membe (11) Wasira (9), Makamba (7),
Magufuli (5), Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (3.3),
Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangala(3.2) na Mwakyembe (2.6).
Katerri alisema utafiti huo pia ulihusu kipengele cha Utawala bora
na vita dhidi ya ufisadi ambapo ulionyesha kuwa Mwigulu Nchemba amepata
asilimia 17.4 ya uwezo wa kupambana na tatizo hilo.
Wengine waliomfuata ni Magufuli (14.2), Membe (11), Lowassa (6.10), Jaji Ramadhani (6) na Mwandosya (5).
Wengine ni Mizengo Pinda (8), Mwakyembe (8), Makamba (7), Samuel Sitta (6), Dk. Kigwangala (3).
Katika kipengele za Uadilifu usiotiliwa shaka katika utumishi
Nchemba alipata asilimia 15, Membe (13), Mwandosya (13), Pinda (8),
Makamba (8) Jaji Ramadhani (7), Lowassa (10%).
Katika kipengele cha hotuba iliyo bora, Katerri alisema Nchemba
alipata alama (A), Wasira( B+), Membe (B+), Mwandosya (B+) Lowassa (B)
na Membe (B). Katerri Alisema lengo la utafiti huo ni kutathmini Elimu
katika Nyanja ya uraia kwa watanzania kupitia vipaumbele katika hotuba
za waliokwisha kutangaza nia kupitia CCM.
Alizitaja wilaya ambako utafiti huo ulifanyika kuwa ni Kinondoni,
Kibaha Vijijini, Kilombero, Rombo, Arumeru, Mbulu na Babati, Lindi,
Mtwara, Njombe mjini, Njombe Vijijini, Mbeya Mjini, Nyamagana,
Biharamulo, Tabora, Nzega, Bahi, Chamwino na Kasulu.
0 comments:
Post a Comment