Katika hukumu hiyo iliyotolewa
mahakama hiyo ime amuru Burkina Faso kuifungua na kuisikiliza upya kesi
hiyo iliyohusisha pia mauaji ya watu wengine watatu.
Hukumu hiyo iliyosomwa karibu kwa muda wa saa moja mbele ya jopo
la majaji 10 lilokuwa likiongozwa na Jaji Kiongozi,GERARD NIYUNGEKO,ilimuru pia
serikali ya Burkina Faso kuchukua jukumu la kuwasaka na kuwapata watuhumiwa wa
mauaji hayo.
Mahakama pia imeamuru serikali ya nchi hiyo kuzilipa fidia ya zai
di ya dola za Marekani milioni moja , familia za watu hao waliouawa.
Mahakama hiyo iliielekeza serikali ya Burkina Faso kuhakikisha
kufanya kila linalowezekana kuwafikisha watuhumiwa husika kwenye vyombo vya
sheria ili nao wapa te haki wanayostahili kwa mujibu wa sheria.
Serikali ya Burkina Faso ilifunga jalada la kesi hiyo mwaka 2006
kwa maelezo ya kukosa ushahidi.
0 comments:
Post a Comment