Image
Image

Serikali Mkoani Tanga kuanza operesheni ya kuwakamata viongozi wa vijiji wanao wakingia kifua Majangili na wachimbaji madini.


Serikali Mkoani Tanga imesema itaanza operesheni y a kuwatafuta na kuwakamata na kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa  sheria ,baadhi ya viongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi kata ambao wanadaiwa kuwakingia kifua majangili na wachimbaji madini wanaoingia katika hifadhi za wanyama na kuharibu mazingira.
Onyo  hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Bwana MAGALULA SAID MAGALULA  alipokuwa   akipokea vifaa vya  ujenzi vyenye thamani ya  Shilingi  zaidi ya  Milioni 15 vilivyolewa na Hifadhi ya Taifa -TANAPA-.
Msaada huo wa vifaa ni  utekelezaji wa ahadi ya Wizara ya  Mali asili na Utali i, chini ya kitengo cha ujirani mwema kusaidia ujenzi wa maabara ya Chuo cha Ualimu cha  Serikali,Wilayani Korogwe .
Awali baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema baada ya kufika chuoni hapo walikuta mafunzo yanayotolewa ni stashahada ya kawaida na cheti ndipo Serikali ilipolazimika kuwapeleka wanafuni 270 kwa ajili ya kusomea stashahada ya juu ya Sayansi na Hisabati na kukuta hakuna vitabu katika maabara chakavu iliyopo .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment