UONGOZI wa Coastal Union,Wagosi wa Kaya umeingia mkataba wa miaka
miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja
kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka
Tanzania Bara itakayoanza Agosti.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Uganda, ameingia kandarasi ya kuinoa
Coastal Union jana jijini Tanga mbele ya Katibu Mkuu wa timu hiyo,
Kassim El Siagi na mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter.
Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa
Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa kutokana na umahiri
aliokuwa nao kocha huyo wana imani ataipa mafanikio timu yao katika ligi
kuu msimu ujao.
Mayanja aliwahi kuzifundisha timu za soka za Kiyuvu FC ya Rwanda,timu
ya Mamlaka ya Mapato (URA),Vipers FC ya Bunamwaya na KCC zote za Uganda
amesema kutua kwake Coastal Union kunampa faraja, hivyo atahakikisha
anatoa mchango wake kuipa mafanikio.
Pia alisema mipango yake ni kuhakikisha timu inang’ara katika
michuano ya Ligi Kuu msimu ujao, ikiwa ni pamoja na kubadili aina ya
mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuhirikiana na
wachezaji, mashabiki na uongozi kwenye medani za kitaifa na kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment