Image
Image

Misri yaanza kuvunja jengo la makao makuu ya chama tawala cha zamani cha NDP.


Misri imeanza kuvunja jengo la makao makuu ya Chama tawala cha zamani cha National Democratic lililopo kwenye uwanja wa Tahriri mjini Cairo, ambako miaka minne iliyopita maandamano makubwa yalimaliza utawala wa miongo kadhaa wa rais wa zamani Hosni Mubarak.
Baraza la mawaziri lilitoa uamuzi wa kuvunja makao makuu hayo mwezi Aprili na baadaye serikali ikatangaza kuvunja jengo hilo lenye ghorofa 15, ambalo lilichomwa moto na waandamanaji walioipinga serikali mwaka 2011.
Ragab Hafez ni mhandisi anayevunja jengo hilo.
"Nimeambiwa nivunje jengo hili ndani ya miezi mitatu, tutakapomaliza ndio tutaanza hatua ya pili ya kubadilisha sehemu hii kuwa bustani."
Chama cha NDP kilivunjwa Aprili 2011 na mali zake zikazuiwa na taifa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment