Bw. Djinnit ataendelea kuwa
mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye kanda ya Maziwa Makuu. Upinzani
umemlaani Bw. Djinnit kwa kupendelea upande wa serikali ya Burundi kwenye mazungumzo
ya pande mbili kuhusu mgogoro uliotokana na rais Pierre Nkurunziza kutaka
kuwania urais kwa awamu ya tatu,Bw. Djinnit amekanusha lawama hiyo.
Habari nyingine kutoka
Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa zinasema, zaidi ya wakimbizi 7,700
wa Burundi wameingia Uganda kuanzia mwezi Novemba mwaka jana, na tangu tarehe
mosi mwezi huu kila siku kuna takriban wakimbizi 144 wanaomiminika nchini
Uganda kutoka Burundi.
0 comments:
Post a Comment