Ripoti hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ukanda huo, UNOCA, Abdoulaye Bathily aliyotoa alipohutubia baraza hilo akisema mashambulio hayo yanaleta matatizo kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati na hata Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Bwana Bathily amesema tangu ripoti yake mbele ya baraza hilo mwezi Novemba mwaka jana, hali imezidi kudorora kila uchao na kutia hofu.
“Nchi za Afrika ya Kati imeingia katika ng'we ya uchaguzi inayomalizika mwaka 2018. Mvutano wa kisiasa kuelekea chaguzi unaongezeka kwenye baadhi ya nchi. Masuala ya marekebisho ya katiba kuhusiana na ukomo wa uongozi yanagawa wapiga kura. Mivutano iandamanayo na ghasia na kusababisha vifo mathalani DR Congo na Burundi. Malalamiki ya kijamii yanashika kasi, yakichochewa na kunywea kwa uchumi kwenye ukanda huo hasa nchi zinazozalisha mafuta."Kufuatia taarifa hiyo, Baraza la usalama limepitisha taarifa inayoshutumu mashambulio likisema yanasikitisha na kwamba yanaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Halikadhalika baraza limeeleza wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa vitendo vya kigaidi vinavyochochewa na kundi la kigaidi la Boko Haram.
0 comments:
Post a Comment