Image
Image

Ni wakati wa kukabiliana na vyanzo vya taabu ya wahamiaji- Ruecker.


Rais wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Joachim Ruecker, amesema kuwa sasa ndio wakati wa kukabiliana na vyanzo vya taabu wanayokumbana nayo wahamiaji, akisema suala hilo na mengine yasiyopewa kipaumbele, yatakuwa miongoni mwa yale yatakayomulikwa kwenye kikao kijacho cha baraza hilo.Bwana Ruecker amesema anatarajia wanachama wa baraza hilo kupitisha pendekezo la Muungano wa nchi za Ulaya, EU, la kujadili suala hilo mnamo Jumatatu mchana, ili liwe miongoni mwa mambo yatakayotangulia kikao hicho kitakapong'oa nanga.
Ameongeza kuwa suala la wahamiaji ni tatizo kubwa kwa nchi wanakotoka, wanakopitia na wanakohamia, akisema ni wakati wa kukabiliana na vyanzo vyake
 "Hakuna yeyote ambaye haki yake imelindwa dhidi ya kufungwa kiholela, dhidi ya utesaji, wala hakuna mtu yeyote anayepata chakula cha kutosha na maji, au asiyekumbana na ukosefu wa ajira, kwa kifupi, hakuna mtu yeyote ambaye haki zake za msingi zimeheshimiwa, angeweza kuweka maisha yake kwenye safari hatarishi na za kutisha, kama wahamiaji hawa wanavyofanya."
Mjadala huo wa Jumatatu unatarajiwa kuyajumuisha pia mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile lile la Wakimbizi, UNHCR, lile la Ajira Duniani, ILO, lile la Afya, WHO, pamoja na wadau

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment