Image
Image

Mkazi wa kijiji cha Mpandapanda anashikiliwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma za kujiandikisha mara mbili daftari la wapiga kura.


Mkazi wa Kijiji cha Mpandapanda Kata ya Kiwira wilayani Rungwe, anahojiwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma za kujiandikisha mara mbili katika Daftari la Kudumu la Wapigakura. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe, Veronica Kessy alisema jana kuwa tayari suala hilo limefikishwa katika vyombo vya sheria.
“Suala hilo kweli lipo lakini siwezi kuzungumza chochote kwani tulishalifikisha kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na linafanyiwa kazi,” alisema Kessy.
Kwa mujibu wa mitandao, mtuhumiwa alikamatwa akiwa na vitambulisho viwili vilivyotolewa kwenye vituo viwili tofauti katika Kijiji cha Mpandapanda.
Kitambulisho cha kwanza kinataja jina la Veklene B. Mwankenja kikionyesha alizaliwa Aprili 26, 1993 alichokipata katika Kituo cha Shule ya Msingi Kiwira A, akiwa amevalia shati la mistari. Lakini kitambulisho cha pili kina jina la Vekline B. Mwankenja akiwa amezaliwa Julai 26, 1996 akiwa amevaa shati na sweta, alichokipata katika Kituo cha Shule ya Msingi Kiwira B.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kijana huyo alikamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
“Alishakamatwa na amefikishwa mahakamani kwa kosa hilo,” alisema Kamanda Msangi.
Baadhi ya wakazi wa Kiwira walipoulizwa kuhusu kijana huyo alipo kwa sasa, walidai kuwa hawajamuona licha ya kusikia taarifa za kukamatwa kwake.
“Huyu mtu hatujamuona tangu atuhumiwe kwa kosa hilo,” alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Kijalo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment