Mkurugenzi mkuu wa Twitter,
Dick Costolo, ana nia ya kujiuzulu ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Juni,
kufuatia shinikizo kutoka kwa wawekezaji, ambao wanalalamikia ukuaji polepole
wa mtandao huo wa kijamii.
Twitter imeshindwa kupata
faida katika kipindi cha miaka tisa tangu ilipoanzishwa.
Mwanzilisho mwenza wa mtandao
huo Jack Dorsey atachukua mahala pake kama kaimu afisa mkuu kuanzia Julai mosi
na kukalia wadhfa huo hadi pale mrithi wake atakapochaguliwa.
Bwana Costolo amekuwa
akishinikizwa kujiuzulu na wawekezaji ambao hawafurahikii ukuwaji wa kampuni
hiyo.
Katika taarifa yake bwana
Costolo amesema kuwa anafurahishwa na wafanyikazi wa kampuni hiyo.
Mnamo mwezi Aprili kampuni
hiyo ilipata hasara ya dola milioni 162.
Bei ya hisa zake ilishuka kwa
asilimia 30 na sasa zinaendelea kuuzwa kwa bei ya uanzilishi wake mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment