Image
Image

Mkutano wa AU kushughulikia hali ya CAR.


Viongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamesema kuwa wanatarajia kwamba mkutano wa viongozi wa Afrika wanaokutana kesho nchini Afrika Kusini ni fursa nzuri itakayosaidia juhudi za kurejesha amani kamili katika nchi hiyo.
Ujumbe wa Jamhuri ya Afrika ya Kati unaoongozwa na Rais wa mpito wa nchi hiyo Catherine Samba-Panza huko Afrika Kusini na unafanya jitihada za kupata msaada wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya kuitisha uchaguzi mkuu nchini humo. Waziri Mshauri katika Masuala ya Ulinzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Marie Noƫlle Koyara, amewaambia waandishi habari kwamba Umoja wa Mataifa umenzisha mchakato wa zoezi la uchaguzi mkuu katika nchi hiyo lakini amesisitiza kuwa msaada wa Umoja wa Afrika una umuhimu mkubwa kwa ajili ya kukomesha kipindi cha mpito.
Maafisa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanasisitiza sana juu ya masuala ya kupokonywa silaha wapiganaji wa makundi hasimu na ujenzi mpya wa nchi hiyo iliyoathiriwa mno na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Chaguzi za Rais na Bunge katika Jamhuri ya Afrika ya Kati zimepangwa kufanyika Juni na Agosti mwaka huu wa 2015.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment