Afisa
wa Wizara ya Afya katika Jimbo la Rivers State DR. SIMEON IBUFUBARA MANEUL
amesema watu hao wamekufa tangu tarehe 31 ya mwezi uliopita na kwamba watu 38
wamekufa baada ya Jumanne wiki hii wakati maafisa walipopiga marufuku
utengenezaji na unywaji wa pombe hiyo ya kienyeji inayoitwa Ogogoro.
Pombe
hiyo hutengenezwa kwa utomvu wa miti ya mitende kama tembo lakini kwa kawaida
huchakachuliwa kwa kuwekwa ethanol
inayoongeza ukali wa p ombe kufikia
viwango vya asilimia 60.
Maafisa
wa afya wanasema mamia ya watu hufa kila mwaka kwa aina ya pombe hiyo na kwamba
mlipuko wa vifo vya hivi karibuni ulianza wakati wa sherehe kwenye mgahawa
mmoja unafahamika sana kwa supu ya mbwa.
0 comments:
Post a Comment