Kiongozi
wa Kanisa Katoliki Duniani Pope FRANCIS amesema anapanga kutembelea Jamhuri ya
Afrika ya Kati na Uganda mwezi Novemba.
Pia
anatumaini kwenda Kenya wakati wa ziara yake hiyo ya kwanza ya Afrika tangu awe
kiongozi wa dunia wa kanisa hilo.
Akizungumza
na kundi la mapadri kutoka kote duniani alisema alikuwa anataka kuongeza Kenya
katika ziara yake hiyo ya Afrika lakini bado iko katika hati hati kwa sababu za
matatizo ya maandalizi.
Hata
hivyo hakuelezea zaidi juu ya magumu ya kutembelea kutembelea Kenya ambayo
lakini imekuwa inalengwa kwa mashambulio na wapiganaji wa Somalia wa kikundi
cha al-Shabaab.
0 comments:
Post a Comment