Image
Image

Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika wafunguliwa.


Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika umefunguliwa huku ukiwa na na malengo ya kujadili masuala ya kuwawezesha wanawake na maendeleo ya muda mrefu ya bara hilo.
Mkutano huo unatanguliwa na kikao cha kamati ya wajumbe wa kudumu, ambacho kitatoa ripoti kuhusu masuala mbalimbali ambazo zitajadiliwa na wakuu wa nchi utakaofanyika mwanzoni mwa wiki ijayo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni balozi wa Zimbabwe nchini Ethiopia Albert Ranganai Chimbindi amezitaka serikali za Afrika zitekeleze makubaliano yaliyofikiwa kwa ajili ya kutimiza usawa wa kijinsia.
Naye naibu mwenyekiti wa kamati hiyo Erastus Mwencha ameainisha ajenda muhimu za mkutano huo zikiwemo kuboresha uchumi wa bara, kuendeleza miundo mbinu, kupunguza umaskini na kulinda amani na usalama.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment