Image
Image

Taasisi ya chakula na lishe imesema idadi ya vifo kwa waathirika wa virus vya ukimwi imepungua.



Taasisi ya chakula na lishe  imesema idadi ya vifo kwa waathirika wa virus vya ukimwi katika mikoa ya Sindgida Arusha na Dodoma imepungua baada ya waathirika kupewa msaada wa tiba lishe  na kupunguza tatizo la utapia mlo.
Akizungumza mkoani Morogoro wadau wa mashirika yanayohudumia waathirika wa virus vya ukimwi wamesema mradi wakutoa tiba lishe kwa waathirika w avirus vya ukimwi 
 chini ya ufadhili wa Global fundi umeonyesha mafanikio kwa baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelalala kitandani ambapo kwa kuwapatia  virutubisho vya tiba lishe waathirika  afya zao zimeboreka na wanaweza kufanya kazi za kuongeza kipato kwa familia.
Nae kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa morogoro Dr.Samson Tarimo amesema kwa mkoa wa morogoro zaidi ya asilimia 44 ya watoto chini ya umri wamiaka mitano wanatatizo la utapia mlo ingawa kunamahusino makubwa kati ya utapia mlo  kwa watu wanaoishi na virus vya ukimwi ambapo kurugenzi wa afya na lishe Dr. Sabas Kimboka amesema kwa miaka minne mradi huu wa kutoa tiba lishe umeanzia katika miko ya singida arusha na dodoma hii inatokana na  kiwango kikubwa cha maabukizi na hali duni ya lishe na wanatarajia kuanzisha mradi  katika mikoa ya tanga mtwara na lindi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment