Watu ishirini wanaosadikiwa
kuwa wahamiaji kutoka nchi jirani wamekamatwa mkoani kigoma baada ya
kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura, katika uandikishaji
wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kielektronik BVR unaoendelea mkoani kigoma.
Mkuu wa mkoa wa kigoma Luten
Kanal mstaafu Issa Machibya amesema wakati wa ibada ya kanisa la kiinjili la
kilutheri tanzania mission ya kigoma iliyoambatana na harambee ya ujenzi wa
shule ya msingi ya kanisa hilo mjini kigoma, kuwa watu hao ambao wamejaribu
kujiandikisha tayari wamefikishwa mahakamani.
Kutokana na hali hiyo ametoa
onyo na kuahidi kuwachukulia hatua kali zaidi ikiwa ni pomoja na
watanzania watakaobainika kuwasaidia wahamiaji kujiandikisha.
Kwa upande
wake askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri tanzania KKKT
nchini DR ELEX MALASUSA amesema moja ya kazi za kanisa
hilo ni kuhakikisha jamii inaelimika na kufuata mafundisho ya mwenyezi mungu
ambapo akizungumzia ujio wa wakimbizi kutoka burundi ametaka wasaidiwe ikiwa ni
pamoja na kuiombea nchi hiyo ili ipate amani.
Katika harambee hiyo
ya ujenzi wa shule ya msingi, zaidi ya shilingi milioni 53 ikiwa ni pesa
taslimu na ahadi zimepatikana.
0 comments:
Post a Comment