Ugonjwa huu huweza kusambaa zaidi endapo kinga ya mwili inakuwa ni ndogo, hivyo makundi ambayo yanaweza kuwa katika hatari ni pamoja na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Kimsingi ili kuzuia maambukizi kwa mtoto mzazi au mlezi ndio anajukumu hilo zaidi na mambo yakufanya ni kama haya yafuatayo:
Mzazi/ mlezi unapaswa kuhakikisha hautumia sabuni zenye kemikali kali ambazo huweza kuchangia muwasho na kusababisha michubuko sehemu za siri. Jambo ambalo huweza kuchangia zaidi maambukizi ya vimelea vya magonjwa ya mfumo wa mkojo.
Aidha, mlezi au mzazi unapaswa kuhakikisha mtoto anakunywa maji yakutosha kila siku.
Kwa wale wenye watoto wakike, wanapaswa kumsafisha mtoto wa kike sehemu ya siri kwa kutoka mbele kwenda nyuma ili kuepuka kuhamisha bacteria wa njia ya haja kubwa ambao kwa kawaida wakitoka katika njia ya haja kubwa kwenda kwenda katika njia ya haja ya mkojo huchangia kusababisha ugonjwa katika mfumo wa mkojo.
0 comments:
Post a Comment