Image
Image

Rais wa TFF Jamal Malinzi aitaka timu ya toto kumaliza mgogoro wao.


Rais wa shirikisho la soka nchini ( TFF ), JAMAL MALINZI amewataka viongozi wa timu ya toto AFRICAN ya jijini Mwanza kukaa pamoja na uongozi wa serikali mkoani humo ili kumaliza mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya klabu hiyo ambao unatishia timu kufanya vibaya katika ligi kuu ya vodacom tanzania bara msimu wa 2015/2016.
MALINZI ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 13 kutoka mikoa 27 ya kisoka ya Tanzania bara, ikiwemo timu ya alliance sports academy kama mkoa mwalikwa ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuchagua timu ya vijana watakaoshiriki mashindano ya vijana ya afrika ( AFCON 2019 ) ambapo Tanzania itakuwa ni mwenyeji wa fainali hizo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano hayo katika uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza mbali na kuitaka kamati ya ufundi kutenda haki kwa kuchagua wachezaji watakaopeperusha vyema bendera ya Tanzania katika fainali za AFCON 2019, pia amegusia Mgogoro wa timu ya toto AFRICAN.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment