Image
Image

Mrembo Sitti: Nilitaka kujiua.


“Nilitaka kujiua kwa njia yoyote ambayo ningeona inafaa, lakini nilirudisha moyo nyuma kwa sababu ingekuwa shida kubwa nyumbani.” Hayo ni maneno ya aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu aliyeamua kulitema taji hilo la ulimbwende baada ya kubebeshwa kashfa za udanganyifu wa umri wakati akishiriki mashindano hayo.
Aliongeza: “Sikuwa na amani, niliishi maisha ya hofu, kujifungia ndani, kulia wakati wote. Ilifikia hatua baba yangu alipata mshktuko kiasi cha kwenda kutibiwa Afrika Kusini. Mama yangu pia alipata mshtuko...ningeweza kumpoteza.”
Anazikumbuka siku 30 za majonzi na maumivu, ambazo kwa kiasi kikubwa zilimuathiri mama yake mzazi ambaye ndoto za binti yake kwenye mashindano ya urembo zilifika tamati.
“Mama yangu alisali na mimi, alinipigania, hakuonyesha hadharani jinsi gani anaumia, lakini ukweli ni kwamba nilimwona alivyokuwa anadhoofu na kukosa raha. Nyumba yetu iligeuka sehemu ya huzuni, amani ilitoweka ni kama tulikuwa na msiba.”
Sitti anasema siku moja mama yake alimwambia: “Sitti mwanangu, nilipompoteza mama yangu nililia na kuumia sana, lakini machungu ninayoyasikia sasa na utu uzima wangu ni mazito.”
“Sikutamani kumwona mama yangu analia, iliniuma na hata sasa nawaza machungu na maumivu aliyopitia kwa ajili yangu,” anasema na kuongeza: “Asichokijua mama, siku moja nilikuwa natoka chumbani kwangu nikimwangalia mama akiwa na gazeti lililokuwa na habari yangu. Nilishikwa na uchungu na kurudi chumbani, niliona kama vile dunia imeniangukia.”
“Wakati huo wote baba yangu alivumilia bila kuonyesha maumivu yake, daima alikuwa mtulivu na japo alipinga vikali mimi kushiriki Miss Tanzania,” anasema Sitti.
Baba aliniambia: “Mwanangu usijali, hivi siyo vita vyako tena, sidhani kama sasa wanakutafuta wewe tena, utabaki kuwa mwanangu.”
Anasema kuna wakati baba yake alikwenda Afrika Kusini na akiwa huko alimtumia ujumbe wa kumuomba msamaha na alimwambia kwamba hizo ni changamoto.
“Aliniambia yeye alikuwa na wasiwasi na mimi, lakini kwa upande wake yupo vizuri, hajawahi kuandikwa sana, lakini kama mzazi ilimuuma sana.”
Sitti anasema alikuwa katika wakati mgumu kiasi cha kufikia uamuzi wa kutupa laini yake ya simu ya zamani.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment