Amesema ni kipindi muhimu kwa kuwa washiriki
wana fursa ya kuchagua iwapo wako tayari kufikia makubaliano baada ya
mapendekezo ya muda mrefu ya kufanyika mwa mkutano huo au wakubaliane kuwa
hawawezi kufikia muafaka na hivyo Libya iendelee na vita.
Hata hivyo amesema kupitia maoni ya baadhi ya
washiriki na wananchi wa Libya, suala la vita halina fursa hivyo mkutano wa
sasa ni fursa ya kuweka historia ya kujenga amani kwa kuzingatia mfungo mtukufu
wa mwezi wa Ramadhani unakaribia ambao ni msimu wa maridhiano na amani.
Kwa mantiki hiyo Leon ambaye pia ni mkuu wa
ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL ametaka wakati wa mfungo, uwe
msimu wa amani na maridhiano, mkusanyiko wa familia uchukue nafasi ya mapigano
na mizozano.
0 comments:
Post a Comment