Watu zaidi ya Elfu-Nane wamekufa wakiwa mikononi mwa Polisi nchini Nigeria katika kipindi cha miaka minne iliyopita
wakati wa mapambano na wapiganaji wa Boko Haram, madai ambayo yamekanushwa
vikali na jeshi.
Shirika la Kimataifa la Kutetea
Haki za Binadamu la Amnesty International linasema walikuwa miongoni mwa zaidi ya watu Elfu-20 walio kamatwa wakati wa oparesheni
za kupambana na wapiganaji wa Boko
Haram.
Kwa mujibu wa shirika hilo watu
wapatao Elfu- 17 wamekufa tangu mwaka
2009,wakati kikundi cha Boko Haram kilipoanzisha
mapambano na serikali, Milioni 1 na Laki- 5 wamekimbia makazi yao na mamia ya wengine kutekwa na
kikundi hicho.
Ripoti hiyo inakuja ,wakati Rais
mpya wa Nigeria na k iongozi wa zamani wa kijeshi wa nchi hiyo Jenerali MUHAMMADU BUHARI ku anza
ziara ya kwanza ya nje nchini Niger,kujadili
oparesheni za kanda dhidi ya kikundi hicho.
0 comments:
Post a Comment