Akifungua mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na
Kilimo endelevu katika nchi za Afrika,(Climate change and Multi-Dimensional
sunstanability in Africa Agriculture),Pro.Molella amesema tafiti hasa za kilimo
zinapaswa kupewa nafasi katika sekta ya kilimo hapa nchini.
Amesema mkutano huo,ambao SUA ndio wenyeji unashirikisha wadau
mbalimbali wa kilimo kutoka nchi za Afrika na watajadiliana fursa ya kilimo
endelevu katika uchumi,jamii na mifumo ya taasisi
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mradi wa Tafiti Bunifu za
Kilimo,(IAGRI)Pro.Isaac Minde amesema katika mradi wao wanafundisha vijana
juu ya namna ya kufanya utafiti katika hali ya ubora zaidi ili kuweza
kupambana na changamoto za kilimo katika maeneo yao,nia ikiwa kuhakikisha
kilimo endelevu kinapata nafasi ya kuinua uchumi wa nchi na namna ya kupambana
na mabadiliko ya hali ya hewa kila msimu wa kilimo.
Naye mdau wa Kilimo,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Paresko Cone,amesema
tafiti zinazofanywa katika kilimo hazina budi kutumika kuisaidia jamii kuweza
kuwa na uwezo wa kuzalisha kila msimu na kuweza kutokomeza njaa ndani ya jamii.
Amesema kinachotakiwa katika sekta ya kilimo ni viongozi
wanaongoza na jamii kuwa wabunifu,kuthubutu,kwani hakun lisilowezekana katika
kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kwani mkoa wa singida wametumia tafiti
za kilimo zilizofanywa SUA na kuzitumia na mpaka sasa mkoa huo una chakula cha
kutosha kwa kila msimu.
Pia amesema mkoa wa singida kwa sasa hakuna tena migogoro ya ardhi
kutokana na mkoa huo kuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi,mkulima na
mfugaji wametengewa maeneo yao na hakuna anayemwingilia mwingine katika eneo
alilopangiwa.
0 comments:
Post a Comment