Imesema vituo vya Uandikishaji
vitakuwa kwenye Vitongoji,Mitaa na Vijiji katika Kata zote za Mikoa hiyo minane
na wale wote waliotimiza masharti wanahimizwa kwenda kujiandikisha.
Taarifa iliyotolewa na tume hiyo
imesema waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatakiwa kujiandikisha ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za
kupigia kura kwa ni kadi za zamani
hazitatumika kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu .
Wananchi wanatakiwa kwenda
kujiandikisha kwenye vituo vya kujiandikisha vilivyoko ndani ya Kata zao na
uandikishaji utaf anyika kwa muda wa
siku saba kwa kila kituo.
0 comments:
Post a Comment