Fan Changlong amesema, rais Xi Jinping wa China
atafanya ziara nchini Marekani mwezi Septemba mwaka huu, na hili ni jambo
muhimu katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa mwaka huu. Ameongeza kuwa
ziara yake hiyo inalenga kutimiza maoni muhimu ya pamoja ya viongozi wa nchi
hizo mbili na kuhimiza uhusiano kati ya majeshi ya China na Marekani uendelezwe
kwa utulivu. Kuhusu suala la Bahari ya Kusini ya China, Fan Changlong ameihimiza
Marekani iendelee na msimamo wa kutounga mkono upande wowote, kupunguza
shughuli za kijeshi kwenye eneo la Bahari hiyo, kushughulikia masuala kwa haki,
na kutofanya mambo yanayoharibu uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili na
kuathiri amani na utulivu wa kikanda.
Kwa upande wake, Carter amesema suala la Bahari ya
Kusini ya China si suala lililopo kati ya China na Marekani, na Marekani
haitaunga mkono upande wowote kwenye mvutano wa mamlaka ya Bahari hiyo,
vilevile imezitaka pande husika zifanye mazungumzo ili kutatua suala hilo kwa
njia ya amani.
0 comments:
Post a Comment