Mbabazi ameibuka kuwa mpinzani mkubwa dhidi ya rais
wa sasa wa Uganda Yower Museveni, ambaye alifanya naye kazi kwa zaidi ya miaka
40. Rais Museveni alimfukuza kazi Mbabazi mwaka jana baada ya ripoti kutoka
chama cha NRM kuwa waziri mkuu huyo anawania nafasi ya juu zaidi ya uongozi
nchini humo. Mbabazi pia alifutwa wadhifa wa katibu mkuu wa chama hicho.
Uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Februari mwaka ujao
nchini Uganda, huku wabunge wa chama tawala cha NRM tayari wamemchagua rais
Museven kugombea tena nafasi hiyo akiwa mgombea pekee wa urais.
Rais Museveni ameshika madaraka hayo tangu mwaka
1986.
0 comments:
Post a Comment