Image
Image

Pinda: Mungu pekee anamjua Rais ajaye.



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alitangaza “kimya kimya” nia ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM, jana alichukua fomu kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, akisema “ni Mungu pekee ambaye anamjua Rais” wa Serikali ya Awamu ya Tano. Pinda, ambaye ameshikilia nafasi hiyo kwa takriban miaka minane, hakutaka kutaja vipa umbele vyake kwa kuwa CCM haijatoa Ilani ya Uchaguzi, lakini akasema katika kikao chake kifupi na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu kuwa iwapo atapewa fursa ya kuongoza nchi, “piga geuza nitahakikisha uchumi wa wanyonge unainuka”.
Pinda anakuwa kada wa 31 kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa na chama chake, kupitishwa kuwania nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini.
CCM itahitimisha uchukuaji huo Julai 2 saa 10:00 jioni na makada wote waliochukua fomu hizo watatakiwa kuwa wamerudisha fomu zilizojazwa na wadhamini kutoka mikoa 15 nchini.
Akizungumza jana mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Pinda alisema ingawa kati ya wote waliochukua fomu kila mmoja anataka apitishwe, Mungu pekee ndiye anayemjua Rais wa Tanzania.
“Mimi simjui, na wala wenzangu hawamjui na kila mmoja anasema moyoni mwake kwamba atakuwa yeye, lakini ni Mungu tu ndiye anayemjua,” alisema.
Pinda alisema hawezi kusema lolote kuhusu vipaumbele vyake, hadi hapo Ilani ya Uchaguzi itakapopitishwa na Mkutano Mkuu wa chama chake.
Hata hivyo, alisema ana uhakika hawezi kushindwa kutekeleza Ilani ya CCM.
“Ilani ndiyo itakayoeleza sera, maelezo na mikakati yote, kwa hiyo sina cha kusema mpaka itakapopitishwa na ikitokea nikateuliwa sitashindwa kuitekeleza na nalisema hili kwa uhakika,” alisema Pinda mbele ya waandishi na wanachama wachache waliohudhuria shughuli hiyo kwenye ukumbi wa ofisi za makao makuu ya CCM mjini hapa.
Pinda alisema amefanya kazi na marais wa awamu zote kuanzia Serikali ya Mwalimu Nyerere na kwamba amejifunza mengi.
Alisema pia amekuwa Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka minane akiwa ndiye msimamizi mkuu wa utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Alisema Rais Jakaya Kikwete amefanya mambo mengi ikiwemo kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo inayoishia mwaka 2025 dira iliyoasisiwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment