Image
Image

Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein amechukua fomu ya kuwania Urais.


Hatimaye Rais wa Zanzibar na  mwenyekiti wa baraza la mapindui Dr. Ali Mohamed Shein amechukua fomu ya kutaka kuteuliwa kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM huku  akitamba hakuna mgombea wa upinzani  yeyote anayempa  hofu.
Dr.Shein akifutana na mke wake Mama Mwanamwema na baadhi ya wanfamilia  alifika ofisi kuu ya CCM kiswandui na kulakiwa na umati mkubwa wa wana CCM waliofika kumuunga mkono na kukabidhiwa fomu hizo na naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai huku akilipiwa ada ya shlingi milioni moja na mkewe.
Baadaye alizungumza na  viongozi wa ngazi mbali mbali wa chama wa  mikoa yote ya Zanibar  ambapo mbali ya kuwashukuru na kuwahidi kuwatumkia kwa nguvo zote wazanzibar kwa misingi ya sheria na katiba  na kulinda mapinduzi na muungnao na badaaye alizungumza na wandishi wa habri  ambapo amemsmea hawaogopi na wala hatishiki na wagombea urais  wazanzibar kutoka vyama vyingine kwa vile wote anawaweza.
Dr.Shein amesema hawezi kuondoka sasa kwa vile malengo ya serikali yake aliyoyaweka hayajamalizika hivyo anataka kipindi cha pili ili afikie huko na kuwachia wazanzibar mustakabali mzuri wa  nchi ikiwemo masuala ya mafuta,gesi na uchumi. 
Drs shein ambaye anatarajiwa kuwa mgombea pekee wa CCM anakuwa mgombea wa sita kutangaza kuwania urais wa Zanzibar  wengine waliotangaza nia  ni maalim Seif Sharrif  Hamad-CUF,Juma Ali Khatibu -TADEA,Said Soud -AFP,Hamad Rashid-ADC na mgombea wa jahazi asilia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment