Serikali imezitaka Halmashauri
kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha mipaka ya Hifadhi za
Taifa inalindwa na kuheshimiwa ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri
Mkuu - TAMISEMI - AGREY MWANRI ameyasema
hayo alipokuwa akijibu swali la
Mbunge wa Kasulu Mjini , MOSES MACHALI aliyeuliza sababu
zilizokwamisha kushughulikiwa agizo la Waziri Mkuu la kutatua tatizo la
wakulima wa Kasulu wanaolima katika eneo la Kagera Nkanda wanaofukuzwa na
kupigwa kila mwaka kwa agizo la mkuu wa Wilaya ya Kasulu .
Waziri MWANRI amesema agizo la
Waziri Mkuu la kutatua tatizo la wakulima wa Wilaya ya Kasulu , hasa Kijiji cha
Kagera Nkanda li metekelezwa kwa kuwapatia wananchi ardhi katika maeneo mengine
ukiacha eneo la hifadhi.
Serikali imesema viongozi wa siasa wa kuchaguliwa na kuteuliwa pamoja na
watumishi wa umma hawaruhusiwi kuwa viongozi k atika vyama vya ushirika nchni.
Naibu Waziri wa Kilimo ,Chakula
cha Ushirika, GODFREY ZAMBI amelieleza Bunge alipokuwa a kijibu swali la Mbunge wa Karatu ,
Mchungaji ISRAEL NATSE , a liyetaka kujua serikali inatoa kauli gani k
uhusu ushiriki wa viongozi wa siasa
kwenye SACCOS ambao umekuwa na tatizo
kubwa .
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula
cha Ushirika, amesema ili
kukabiliana na matatizo ya ushiriki wa wanasiasa katika uongozi wa
vyama amb ayo imeanza kutumika rasmi
Januari mwaka jana imeainisha mambo mbalimba li ikiwemo kuzuia
viongozi wa siasa na watumishi wa umma
kuwa viongozi wa Vyama vya ushirik a .
Bunge limeelezwa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini
,imeipatia kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources
Limited Leseni ya uchimbaji mkubwa wa
madini ya chuma katika eneo la Liganga.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
,CHARLESS KITWANGA amesema hayo
alipokuwa a kijibu swali la mbunge wa Viti Maalum ,RITA KABATI,a liyetaka kujua
Serikali imefikia wapi katika mkakati wa kuvuna rasilimali ya madini ya chuma ,hasa katika eneo la Liganga Wilayani Lud ewa ili kuendeleza viwanda vya chuma na
kuleta mabadiliko ya viwanda nchini.
0 comments:
Post a Comment